Tundu Lissu aruhusiwa kujiwakilisha mahakamani

  • | Citizen TV
    457 views

    Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ameiambia mahakama kuwa atajiwakilisha mwenyewe kwenye kesi ya uhaini inayomkabili. Lissu ameiambia mahakama kuwa haki zake za kimsingi kupata uwakilishi zimekiukwa na hata budi kujiwakilisha. PIA AMESEMA kuwa amekuwa akichunguzwa na polisi pakubwa huku akizuiliwa kwa wafungwa wa hukumu za kifo. Kiongozi huyu wa upinzani alizuiliwa mwezi Aprili, kwenye hatua iliyoibua upinzani mkubwa kutoka kwa mashirika ya kimataifa kutaka aachiliwe.