Uchaguzi wa serikali za mitaa ubatilishwe na urudiwe.

  • | BBC Swahili
    767 views
    Chama cha upinzani ACT Wazalendo kinataka uchaguzi wa serikali za mitaa ubatilishwe na urudiwe. Madai hayo ni kutokana na kile walichokiita kuharibiwa kwa uchaguzi huo, wakisema uchaguzi uligubikwa na vitendo vingi vya uonevu kwa wagombea na wafuasi wao, ikiwa ni pamoja na uvunjwaji mkubwa wa sheria na kanuni mbalimbali za uchaguzi. Chama hicho kiliambulia chini ya asilimia moja ya kura kwa kila nafasi iliyogombewa huku chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikitangazwa kupata takribani asilimia 97. Kiongozi wa ACT Wazalendo Dorothy Semu amezungumza na mwandishi wa BBC Sammy Awami juu ya msimamo wa chama chao juu ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa. #bbcswahili #tanzania #siasa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw