Uchunguzi wa Mwanablogu wa Meru I Majasusi wa idara ya upelelezi wafunga makao ya gavana Mwangaza

  • | KBC Video
    34 views

    Majasusi wa kitengo cha uchunguzi wa mauaji cha idara ya upelelezi wamefunga makao rasmi ya gavana wa Meru Kawira Mwangaza katika mtaa wa Milimani mjini Meru wakiyataja kuwa eneo la uhalifu. Majasusi hao ni sehemu ya kundi linalochunguza mauaji ya mblogu Daniel Muthiani, al maarufu Sniper. Hattua hiyo inajiri takriban saa 24 baada ya gavana huyo kuvunja kimya chake kuhusiana na mauaji ya mwanaharakati huyo akisema kuwa idara ya ujasusi inafaa kuhitimisha swala hilo na kuwakamata wauaji wake. Na jinsi mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim anavyotuarifu washukiwa watano wanaohusishwa na mauaji ya mblogu huyo wanazuiliwa na polisi huku msako dhidi ya washukiwa wengine wanaohusishwa na kifo chake ukiendelea.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive