Uchunguzi wa umma wa sakata ya figo waanza mbele ya kamati bungeni

  • | Citizen TV
    500 views

    Mbunge wa Nandi hills Bernard Kitur ameiambia kamati ya afya ya bunge la kitaifa kwamba raia wa kigeni walikuwa wanalipa shilingi milioni 30 kupata figo moja nchini. Kitur akisema vijana waliohusishwa na upandikizi wa figo waliahidiwa shilingi laki tano. Akizungumza mbele ya kamati ya afya leo, mbunge huyo sasa anataka waathiriwa, wengi ambao wakiwa wanaugua baada ya upasuaji, kufidiwa.