Ujenzi wa barabara ya Bura kwenda Mwatate katika kaunti ya Taita Taveta wakwama

  • | Citizen TV
    131 views

    Serikali ya kitaifa imetakiwa kurejelea ujenzi wa barabara ya Bura kwenda Mwatate katika kaunti ya Taita Taveta ambayo imekwama kwa zaidi ya miaka minne na ambayo inategemewa zaidi na wakulima sehemu hiyo. Rais William Ruto mwezi wa pili mwaka huu alitangaza kwamba barabara hiyo inayogharimu shilingi bilioni mbili ingeendelea kujengwa ila hadi sasa Mkandarasi bado hajarudi kazini. Julius Joho na maelezo zaidi.