Ujerumani yafanya msako dhidi ya kundi linalodaiwa kuendeleza itikadi za Iran

  • | VOA Swahili
    207 views
    Polisi nchini Ujerumani walivamia maeneo 54 kote nchini katika uchunguzi wa kituo chenye makao yake mjini Hamburg kinachoshukiwa kuendeleza itikadi za Iran na kuunga mkono shughuli za Hezbollah, serikali ilisema Alhamisi. Wizara ya Mambo ya ndani ilisema Kituo cha Kiislamu cha Hamburg, au IZH, kimekuwa chini ya uangalizi wa shirika la kijasusi la ndani la Ujerumani kwa muda mrefu. Ilisema shughuli za kundi hilo zinalenga kueneza "dhana ya kimapinduzi" ya kiongozi mkuu wa Iran. Wizara ya Mambo ya ndani ilisema ujasusi wa Ujerumani unaamini kuwa kuna ushawishi mkubwa au udhibiti kamili juu ya misikiti na vikundi vingine, na kwa mara nyingi wanaendeleza "mtazamo wa wazi wa chuki na dhidi ya Israeli." Ilisema mamlaka inachunguza ikiwa inaweza kupigwa marufuku, na nyenzo zilizokamatwa wakati wa upekuzi zitatathminiwa.