- 394 viewsDuration: 1:29Katibu Mkuu wa Idara ya Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Ahmed Abdisalan Ibrahim, ametembelea eneo la Wajir Kaskazini huku ukame ukiendelea kuathiri wakazi. Akizungumza wakati wa Kutoa chakula cha msaada, Katibu Mkuu huyo alisema serikali inaongeza hatua za kukabiliana na ukame, ikiwemo usafirishaji wa maji kwa magari, kupanua Mpango wa Hunger Safety Net, pamoja na kuongeza mgao wa chakula cha msaada.