Ukarabati wa bwawa la Mwereni waanzishwa na serikali ya kaunti ya Kwale

  • | Citizen TV
    49 views

    Ukarabati wa bwawa la shilingi milioni 78 umeanzishwa na serikali ya kaunti ya Kwale katika eneo la Umoja wodi ya Mwereni eneo bunge la Lungalunga. Bwawa hilo litakalo kuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 230 za maji litakapokamilika litafaidi zaidi ya familia 2,000. Gavana Fatuma Achani amesema bwawa hilo litapunguza uhaba wa maji unaokumba maeneo ya Lungalunga na kuendeleza kilimo cha unyunyizaji mashamba.