Ukosefu wa ajira umeendelea kuhangaisha vijana

  • | Citizen TV
    4,211 views

    Hebu fikiri hili, umesoma chuo kikuu kwa miaka hadi kuhitimu tayari kuanza maisha kama msomi kwenye jamii. Miaka miwili baadaye, maisha yamegeuka bila kazi wala kibarua. Hii ndio hali inayowakumba mamilioni ya wakenya waliomaliza masomo, kwenye hali inayopigiwa darubini na maisha ya vijana watatu kutoka kaunti ya Kisii walioamua kufanya ujenzi wa nyumba za tope angalau kujikimu.