Ukusanyaji wa maoni kuhusu mswada wa nyumba wa 2024

  • | K24 Video
    72 views

    Wanabodaboda katika kaunti ya nakuru wanaitaka serikali kutoa nafasi ya kulipia nyumba za bei nafuu kupitia akiba ya vyama vyao vya ushirika ili kuhakikisha hawawachwi nyuma katika kumiliki nyumba. Kaunti ya Nakuru ina takriban wanabodaboda elfu 52 ambao kupitia wasimamizi wao wamesema iwapo serikali itakubali pendekezo lao basi watahisi ni wadau wa karibu wa mradi huu wa nyumba za bei nafuu. Hayo yamesemwa leo wakati wa ukusanyaji wa maoni ya umma kuhusiana na mswada wa nyumba za bei nafuu.