Ulaghai wa kazi za ng'ambo

  • | Citizen TV
    584 views

    Wakenya waliolaghaiwa pesa kwa ahadi ya kazi za ughaibuni sasa wanalaumu utepetevu wa maafisa wa uchunguzi kuchukua hatua, miaka miwili baadaye. Waathiriwa hawa wakiendelea kukadiria hasara ya mikopo na mali waliyopoteza kwa ahadi hizo. Na sasa wanalalamika kuwa wamiliki wa kampuni iliyohusika na mipango ya safari hizo wameendelea kusalia huru licha ya kuripoti na hata kufikisha kesi mahakamani.