Skip to main content
Skip to main content

Umaarufu wa Kevin Ruhiu waongezeka, akiwakilisha Kenya katika mashindano ya Afrika

  • | Citizen TV
    2,488 views
    Duration: 3:45
    Jina, Kevin Kiarie Ruhiu limeanza kutambulika na Wakenya katika siku za hivi karibuni. Kevin ni mwanariadha ambaye anawakilisha Kenya katika mashindano ya bara Afrika ya mchezo wa tausha yaani skating huko Misri. Tayari ameshinda medali mbili za dhahabu akiwinda ya tatu. Si mara ya kwanza Kevin kuwakilisha Kenya katika rubaa za kimataifa katika mashindano haya ambayo hayana umaarufu sana nchini. Ila Kevin ambaye anafanya mafunzo peke yake, na ambaye anategemea wahisani kugharamia safari zake anajikakamua kuhakikisha Kenya inatambulika duniani katika mchezo huo..