Umma wahamasishwa kuhusu ugonjwa wa kisukari

  • | Citizen TV
    233 views

    Matembezi ya kuhamasisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari yalifanyika jijini Nairobi kwa lengo la kuchangisha fedha na kuwasaidia watoto wanaoishi na aina ya kwanza ya ugonjwa wa kisukari. Matembezi hayo yaliyodhaminiwa na Citizen Digital kwa ushirikiano na wadau wengine, yaliwashirikisha watu mbalimbali waliotembea umbali wa kilomita 12.6. Matembezi hayo yalianzia na kukamilika katika uwanja wa Carnivore. Mpango huo unalenga kuhimiza uchunguzi wa mapema, upatikanaji wa dawa, na udhibiti wa hali hiyo miongoni mwa watoto kutoka jamii zilizoko katika mazingira magumu.Waandalizi walisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika kukabiliana na ongezeko la visa vya kisukari na kusaidia wagonjwa wenye umri mdogo wanaohitaji uangalizi wa mara kwa mara.