'...Unapotoa fursa bora kwa wanaume na wanawake nini kinatokea...'

  • | VOA Swahili
    163 views
    Kila mwaka wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likikutana New York, kuna matukio ya pembeni yanaadaliwa au kudhaminiwa na UN kukiwa na mikutano, mijadala na mihadhara juu ya maudhui mbalimbali yanayohusiana na kikao cha UNGA. Sikiliza rai ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Wizara ya Elimu Kenya Sarah Ruto kuhusu kutoa elimu bora kwa wanaume na wanawake, Moja ya matukio yaliyofanyika pembeni ya kikao cha mwaka huu ilikuwa juu ya maudhui #Achieving #GapZero Evidence- Driven Inclusive Governance in Africa,” iliyoangazia namna na kuongeza ushiriki wa kisiasa wa wanawake katika bara hilo. Tukio hilo lilishirikisha mazungumzo ya ngazi ya juu akiwemo Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, Ahunna Eziakonwa, naibu mkurugenzi wa utawala na kanda wa UNDP Afrika, Colleen Zamba, katibu wa Rais wa Malawi, Abdoulie Janneh, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mo Ibrahim na wengine. #unga #voaunga #unga78