UNGA 78: '...Unapotoa fursa bora kwa wanaume na wanawake nini kinatokea...' Sarah Ruto

  • | VOA Swahili
    0 views
    Kila mwaka wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likikutana New York, kuna matukio ya pembeni yanaadaliwa au kudhaminiwa na UN kukiwa na mikutano, mijadala na mihadhara juu ya maudhui mbalimbali yanayohusiana na kikao cha UNGA. Moja ya matukio yaliyofanyika pembeni ya kikao cha mwaka huu ilikuwa juu ya maudhui "#Achieving #GapZero Evidence- Driven Inclusive Governance in Africa,” iliyoangazia namna na kuongeza ushiriki wa kisiasa wa wanawake katika bara hilo. Tukio hilo lilishirikisha mazungumzo ya ngazi ya juu akiwemo Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, Ahunna Eziakonwa, naibu mkurugenzi wa utawala na kanda wa UNDP Afrika, Colleen Zamba, katibu wa Rais wa Malawi, Abdoulie Janneh, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mo Ibrahim na wengine. Endelea kusikiliza anachoeleza Katibu Mkuu Kiongozi, Wizara ya Elimu Kenya... #unga #marekani #un #umojawamataifa #mafanikio #usawa #voa #voaswahili #marekani #sarahruto #wizarayaelimu #kenya #moibrahim #voaunga #unga78 - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.