- 283 viewsUpasuaji wa miili ya waathiriwa watatu wa maandamano ya kupinga gharama ya juu ya mafuta katika eneo la Molo, Kaunti ya Nakuru, umebaini kuwa wote walifariki kutokana na majeraha ya risasi. Aidha, upasuaji wa miili ya waathiriwa waliopigwa risasi kwenye maandamano ya kupinga kukamatwa kwa kiongozi wa vijana katika Kaunti ya Busia pia umeonyesha kuwa mauaji hayo yalisababishwa na risasi.