Skip to main content
Skip to main content

Upinzani watishia kususia uchaguzi iwapo mageuzi hayatafanywa IEBC

  • | Citizen TV
    1,123 views
    Duration: 3:29
    Tukisalia kwenye siasa na wanasiasa, muungano wa upinzani sasa unasema kuwa utasusía uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027 iwapo mageuzi makubwa hayatafanywa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka - IEBC. Viongozi hao wanataka IEBC kusitisha ushirikiano wake na kampuni ya Smartmatic kuwatambua wapigakura katika uchaguzi ujao, wakisema kampuni hiyo imehusishwa na utata kwenye chaguzi za mataifa mbalimbali. Viongozi hao wanasema mashine hizo huenda zikatumika vibaya na kuathiri matokeo ya uchaguzi.