- 55,762 viewsDuration: 8:36Huduma za usafiri wa umma zimesambaratika katika miji mbalimbali nchini kufuatia mgomo uliosababishwa na ongezeko la bei ya mafuta. Wakenya walikumbwa na taswira isiyokuwa ya kawaida asubuhi ya leo baada ya wahudumu wa magari ya usafiri wa umma kusitisha huduma zao barabarani, hatua ambayo imewaathiri pakubwa wananchi waliokuwa wakielekea katika maeneo mbalimbali.