Usalama barabarani | Serikali yakadiria upya kanuni za ukaguzi wa magari

  • | KBC Video
    13 views

    Serikali inashirikiana na sekta za kibinafsi katika kuboresha usalama wa barabarani kwa kutathmini upya sheria ya mwaka 2023 kuhusu Madereva walevi na ukaguzi wa magari mabovu. Akizungumza wakati wa mkutano wa kutafuta maoni ya umma kwenye Kaunti ya Nairobi, Afisa mkuu wa masuala ya usalama wa barabarani katika halmashauri ya kitaifa kuhusu uchukuzi na usalama barabarani Samuel Musumba, alisema hatua hiyo inafanyika kwa kuzingati mpango wa serikali ya kujidhibiti kwa watu binafsi. Hata hivyo wadau katika sekta ya umma ambao walihudhuria mkutano huo, waliitaka serikali kukabiliana na maderava wanaokiuka sheria za barabarani. Tayari halmashauri ya NTSA imezuru kauti nne ikipokea maoni ya umma, zoezi ambalo litakamilika mwezi machi mwaka huu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #usalamabarabarani #News #NTSA