Ushuru Wa Nyumba: Wafanyakazi wa ujenzi wahofia kupoteza ajira

  • | KBC Video
    65 views

    Baadhi ya wajenzi katika mtaa wa South B, kaunti ya Nairobi wameelezea wasiwasi wao kufuatia uamuzi wa mahakama kuu kwamba ushuru wa nyumba za gharama nafuu ni kinyume cha katiba. Wajenzi hao wanaofanya kazi chini ya mpango wa nyumba za bei nafuu, wameelezea wasiwasi kwamba huenda wakapoteza ajira wakati taifa likishuhuhudia gharama ya juu ya maisha na ukosefu wa ajira. Haya yanajiri huku wizara ya nyumba ikiwaonya waajiri dhidi ya kutowakata wafanyakazi wao ushuru huo na kuuwasilisha kwa KRA ikiashiria kuwa uamuzi wa korti uliahirisha utekelezaji wa maamuzi yake hadi Januari 10 mwaka ujao.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News