Skip to main content
Skip to main content

Utekaji Tanzania: ‘Familia zina maumivu, serikali ipo kimya’

  • | BBC Swahili
    24,163 views
    Duration: 10:07
    Zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Tanzania, inaelezwa kuwa macho ya wengi yanaangazia taifa hilo la Afrika Mashariki na jinsi linavyoshughulika na wakosoaji wake katika kipindi hiki. Taarifa mbalimbali zimekuwa zikitaja kuwa wakosoaji wa Serikali ya Tanzania wamekuwa wakipotezwa au kutekwa huku mamlaka zikiwa kimya. Watetezi wa haki wameeleza kuwa wanaharakati na wanasiasa wa upinzani wamepotea kwa nyakati tofauti huku baadhi hawajaonekana tena, wakati wengine hurudi na simulizi za kutisha. BBC imezungumza na familia zilizoathiriwa na mikasa hiyo inayoendelea kuripotiwa. Serikali ya Tanzania imekanusha kuhusika na matukio ya watu kupotea. BBC ilituma maombi ya mahojiano na polisi lakini haikujibiwa. Taarifa imeandaliwa na Alfred Lasteck. - - #bbcswahili #utekaji #tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw