Uuzaji wa pombe kwa umma wapigwa marufuku, NACADA yapendekeza umri uongezwe hadi 21

  • | Citizen TV
    631 views

    Uuzaji wa pombe kwenye maeneo na maduka ya umma, na hata kuuza vileo kupitia mitandao itakuwa marufuku, endapo mapendekezo mapya ya halmashauri ya kukabiliana na utumizi wa dawa za kulevya nchini yataidhinishwa. Aidha, kwenye mapendekezo haya mapya, NACADA inataka umri wa kuanza kunywa pombe kuongezwa kutoka miaka 18 hadi 21