- 2,725 viewsDuration: 1:58Katika juhudi za kuimarisha utalii na kupanua Uchumi wa Pwani ya Kaskazini, uzinduzi wa uwanja mpya wa ndege wa vipingo utakua na safari mpya za ndege zinazounganisha Nairobi na Vipingo Kaunti ya Kilifi. Hatua hiyo inalenga kuleta nafuu kwa watalii wanaozuru Pwani Kaskazini haswa kaunti ya Kilifi, wamiliki wa nyumba, wawekezaji, wachezaji wa gofu na wasafiri wa kibiashara na kuinua hadhi ya kaunti hiyo kama kitovu cha utalii na uwekezaji.