- 338 viewsDuration: 2:46Huduma za afya hasa ya uzazi zitaboreshwa zaidi kaunti ya Kilifi kufuatia uzindizi wa chumba cha kina mama cha kujifungua chenye vitanda 40 vya kisasa na vyumba vya upasuaji. Akizungumza katika hospitali ya gatuzi ndogo la Malindi wakati wa uzinduzi huo gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung'aro amesema hatua hiyo itazuia pakubwa changamoto inayofungamana na maswala ya uzazi ikiwemo vifo ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa wakati kina mama wanapojifungua. Kulingana na Waziri wa afya kaunti hiyo Peter Mwarogo, chumba hicho ni moja ya mradi unaolenga kuboresha afya ya uzazi kwa kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya na hamasa kwa madaktari wa nyanjani