- 269 viewsDuration: 4:10Kwa miaka mingi, maelfu ya vijana katika kaunti ya Baringo wameishi bila kutambulika rasmi kwa kukosa kitambulisho cha kitaifa. Wengi wakisema upana wa Baringo, ukosefu wa usalama na hali mbaya ya barabara zikiwa miongoni mwa sababu zilizochangia wengi kukosa nafasi hiyo. Lakini sasa, kuna tumaini kwani serikali kupitia idara ya uhamiaji imezindua zoezi la siku kumi la kutoa kitambulisho katika kaunti ya Baringo