- 198 viewsDuration: 2:01Jumuiya ya vijana wa Pwani kutoka Kaunti 6 za ukanda huo imezindua baraza la kuwahamasisha wenzao kujisajili kuwa wapiga kura katika eneo la mwanjama rabai Kaunti ya Kilifi. Kulingana nao, nia yao ni kuwaleta vijana pamoja ili kuwaelimishana kuhusu umuhimu wa kujiandikisha kuwa wapigakura. Afisa wa tume ya IEBC eneo la rabai Hillary kombe, amewarai vijana kujiandikisha kabla ya shughuli hiyo kukamilika jumanne hii.