Vijana na baadhi ya viongozi Kericho wafanya mashauriano ya amani

  • | Citizen TV
    930 views

    Vijana, Wazee na Viongozi wa Kericho Wameandaa Mkutano wa Amani kuadhimisha Siku ya Saba Saba na kutangaza makataa Ya siku 21 Kuhusu kwa serikali kutoa muongozi kwa Vijana Vijana kutoka Kaunti ya Kericho, wakishirikiana na wazee, viongozi wa kidini na Wajumbe watatu wa Bunge la Kaunti waliandaa mkutano wa amani katika bustani ya Moi hapo jana, wakichagua njia ya mazungumzo badala ya maandamano kudai haki zao. Akihutubia mkutano huo, Rais wa Vijana wa Kericho, Elkana Mutai, aliwapongeza vijana kwa kuchagua amani lakini pia alitoa makataa ya siku 21 kwa Gavana Dkt. Erick Mutai, Seneta Aaron Cheruiyot, Wabunge na Wajumbe wa Bunge la Kaunti kuhakikisha utekelezaji wa matakwa ya Katiba kuhusu kutenga asilimia 30 ya kandarasi na zabuni za kaunti kwa vijana, wanawake na watu walemavu.