Skip to main content
Skip to main content

Vijana wataka kansa itangazwe kuwa janga la taifa

  • | Citizen TV
    1,705 views
    Duration: 1:27
    Mamia ya vijana kutoka kaunti ya Kitui na ukambani wameanzisha kampeni ya kutaka maradhi sugu ya saratani kutangazwa kuwa janga la kitaifa nchini. Kulingana na mwasisi wa kampeni hiyo vijana hao walilazimika kutembea zaidi ya kilomita 160 hadi Nairobi kuwasilisha malalamishi yao katika afisi ya rais iliyoko kwenye jumba la Harambee kutaka saratani kutajwa janga . Hatua hii iliafikiwa baada ya idadi kubwa ya wakenya kuangamizwa na jinamizi la saratani huku wengi wakisalia maskini kutokana na gharama ya juu ya matibabu.