Vijiji kadhaa vyafunikwa na maji Ugiriki baada ya kumalizika kwa janga la moto liliosababisha maafa

  • | VOA Swahili
    398 views
    Mvua kubwa inayonyesha kwa siku tatu mfululizo, baada ya kuzimika kwa moto mkali uliosababisha maafa makubwa kaskazini mwa Ugiriki, imevigeuza vijiji kadha kuwa ziwa katika nyanda ya Thessaly. Maafisa wametuma wapiga mbizi na wataalmu wa kuwaokoa watu ndani ya maji wakati wakazi wa maeneo yaliyoathirika vibaya kupanda juu ya mapaa ya nyumba zao kupata hifadhi. Maji ya mafuriko yanaripotiwa kupandana hadi futi mbili katika baadhi ya maeneo. Idara ya zima moto inasema imewaokoa karibu watu 820 tangu siku ya Jumanne. Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis ameahirisha kutoa hotuba ya kila mwaka juu ya hali ya uchumi iliyopangwa mwishoni mwa wiki hii na badala yake atatembelea maeneo yaliyohabiriwa na mvua akisema nchi inakabiliwa na siku tatu za hali ya maajabu ambayo ahijawahi kusuhudiwa. Mafuriko kutokana na dhoruba Daniel yameathiri nchi jirani za Bulgaria na uturuki na karibu watu 15 wamefariki katika nchi hizo tatu. Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari #mvua #mafuriko #ugiriki #janga #moto #maafa #voa #voaswahili #dunianileo - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.