Viongozi Kisii wahimiza mazungumzo na madaktari

  • | Citizen TV
    422 views

    Viongozi wa kaunti ya Kisii wamesikitikia hali katika hospitali mbalimbali nchini kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea kulemaza utoaji wa huduma za afya kwa siku ya 16 sasa. Viongozi hao akiwemo mwakilishi wa kike wa kaunti hiyo Dorice Aburi walikuwa wakizungumza katika eneo la Bobaracho kwenye hafla ya kuwasaidia wasiojiweza msimu huu wa pasaka.