Viongozi wa magharibi wapinga ukodishaji wa viwanda

  • | Citizen TV
    272 views

    Tetesi zinazidi kuibuliwa kuhusiana na ukodishaji wa viwanda vinne vya sukari huku baadhi ya wabunge kutoka eneo la magharibi wakipinga vikali hatua hiyo na kusema kuwa italemeza uchumi wa wakazi wa magharibi. Wabunge hao wameshangaa ni vipi kiwanda cha Nzoia kilikabishiwa mfanyibiashara Jaswant Rai ilhali mahakama iliamrisha mchakato wa ukodishaji usimamishwe. Wabunge hao wanasema mwekezaji huyo huyo alichukua usukani wa kiwanda cha Panpaper na kutoa ahadi ya kukifufua, ila hadi sasa hajafanya hivyo.