- 169 viewsViongozi wa makanisa wameendelea kuwaonya wanasiasa kukoma kuendeleza siasa za matusi na kudhalilishana kama ilivyoshuhudiwa siku chache zilizopita. Viongozi hawa wakijumuishwa askofu wa kanisa katoliki jimbo la Nyeri Anthony Muheria na mwenzake wa Nairobi Phillip Anyolo wamesema, siasa hizi zinahatarisha taifa.