Viongozi wa Mandera waunga hatua ya TSC kuwafuta kazi walimu waliosusia kazi

  • | Citizen TV
    216 views

    Viongozi wa kaunti ya Mandera wameunga mkono hatua ya tume ya walimu TSC kuwafuta kazi walimu waliosusia kazi wakisaka uhamisho kutokana na ukosefu wa usalama. Gavana wa kaunti hiyo Mohammed Khalif amesema kuwa sekta ya elimu imelemazwa kabisa kaunti hiyo kutokana na hali hiyo. Inahofiwa kuwa wanafunzi wanaotarajiwa kuanza mitihani ya kitaifa kuanzia wiki ijayo wameathirika pakubwa na ukosefu wa walimu. Gavana Khalif anawahimiza wakazi kujiunga na taasisi za mafunzo ya ualimu ili kuinua viwango vya elimu kaunti hiyo