Viongozi wa muungano wa Azimio wakutana kwa mara ya kwanza

  • | K24 Video
    177 views

    Muungano wa Azimio umeelezea masikitiko yake kuhusu kudorora kwa uchumi, sekta ya elimu, ongezeko la ushuru,na kulemaa kwa vita dhidi ya ufisadi. Muungano huo ambao ulijitokeza kwa mara ya kwanza ukiwa na vinara wote kwa pamoja ,umekanusha madai ya kusambaritika ,na sasa unashikilia kuwa unatafuta mbinu mpya ya kushinikiza serikali ya kenya kusikiza kilio cha wakenya. Azimio aidha imeonya taifa la marekani dhidi ya kuingilia masuala ya taifa hasa kuhusiana na kesi ya haiti. Vyama tanzu vya muungano vimetakiwa vianzishe mikakati ya kujizolea umaarufu ili kuupa muungano nguvu.