- 1,386 viewsDuration: 1:57Viongozi wa chama cha ODM kaunti ya Taita Taveta wamesema wako tayari kwa uchaguzi wa chama hicho katika ngazi ya kaunti baada ya mahakama ya kutatua migogoro ya vyama vya kisiasa kusema uchaguzi uliofanyika mwaka jana urejelewe. Aidha viongozi hao wamesema hawako tayari kwa uteuzi wa makubaliano na baadhi ya wanachama bali wanataka uchaguzi. Kulingana nao, ODM kitakuwa na wagombea katika nyadhifa mbalimbali licha ya baadhi yao kupendekeza maridhiano na vyama vingine vya kisiasa.