Vita dhidi ya ufisadi katika serikali za kaunti

  • | K24 Video
    17 views

    Tume ya maadili na kupambana na ufisadi , EACC imezipa serikali zote za kaunti muda wa siku 60 kuwasilisha mpango wa jinsi zitakavyoanzisha ukaguzi wa ndani wa mahesabu wenye ufanisi ndani ya kaunti hizo. Kwa mujibu wa EACC , hiyo ni sehemu ya mkakati wao wa kumaliza ufisadi kwa kushughulikia mifumo inayotoa nafasi ya kupora na ubadhirifu wa rasilimali za umma. Tume hiyo pia imekanusha kuwa na upendeleo wa kisiasa katika vita dhidi ya ufisadi.