Vita vyachacha katika bunge la Machakos

  • | Citizen TV
    1,726 views

    Taharuki na kizaazaa kilishuhudiwa leo katika bunge la kaunti ya Machakos na lile la Homa Bay kufuatia mizozo ya uongozi kwenye mabunge hayo. Katika bunge la Machakos, vita vilizuka huku wawakilishi wakirushiana makonde saa chache baada ya shughuli za bunge kurejelea vikao vyake mapema leo. Wawakilishi wodi 9 sasa wakitimuliwa kwa zogo hili. Wakati huo huo, fujo pia limeshuhudiwa kaunti ya Homa Bay kwenye utata kuhusu kiongozi wa wengi.