Vita: Wachambuzi wa kisiasa na ulinzi waeleza nini lengo la Putin
Wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wakijiandaa kwa mazungumzo ya dharura kuhusu misaada ya kijeshi baada ya utawala wa Trump kusitisha msaada wake kwa Ukraine, wataalam kadhaa wa Russia wanasema kuwa Moscow inajitahidi kuvuruga mshikamano wa Magharibi.
Kufuatia majibizano ya wiki iliyopita huko White House kati ya viongozi wa Marekani na wale wa Ukraine, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, Jumatatu aliilaumu Ulaya kwa kuendeleza vita hivyo, akiongeza kuwa marekebisho kwenye sera za mambo ya nje za Marekani kwa sehemu kubwa zinaendana na mtazamo wa Moscow.
Maoni hayo yamekuja kabla ya kuanza kwa mkutano wa fedha wa Umoja wa Ulaya Alhamisi ukilenga kuimarisha usalama wa bara hilo pamoja na msaada kwa Ukraine ambayo kwa miongo kadhaa imekuwa ikitegemea msaada wa ulinzi kutoka Marekani.
Kwenye mahojiano ya hivi karibuni na gazeti la kijeshi la Krasnaya Zvezda, Waziri wa Mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov alimtaja rais Trump kama “ mtu anayeangalia masuala kwa kina” na kwamba kauli mbiu yake ni “tumia akili.” Alisema kwamba majanga yote ya dunia kwa zaidi ya miaka 500 iliyopita yalianzia au kufanyika Ulaya kutokana na sera zao wakati Marekani ikiwa haijahusika.
#trump #zelenskyy #ukraine #russia #voa #makamurais #jdvance #msaada
4 Aug 2025
- The warning comes amid complaints from Kenyans.
4 Aug 2025
- Harambee Stars secured their first-ever victory at CHAN on Sunday.
4 Aug 2025
- The pair was charged a day after their arrest.
5 Aug 2025
- Enquiries revealed that two plots were used as collateral to acquire a loan on which the borrowers defaulted.
5 Aug 2025
- Education Cabinet Secretary Julius Ogamba finds himself increasingly sidelined by his own Principal Secretaries.
5 Aug 2025
- Why US ballooning public debt is a key concern for Kenya
5 Aug 2025
- Nairobi Expressway contractor to shoulder Sh6.9b tax bill
5 Aug 2025
- Court spells the end of Isiolo's 60-year-old bar, a relic of 'choma'
5 Aug 2025
- Kebs deal with Japanese firm for car inspections under scrutiny
5 Aug 2025
- Why civil society wants Hustler Fund scrapped
5 Aug 2025
- Will Kenya Kwanza's scorecard be enough to win Ruto a second term?
5 Aug 2025
- Kenyan athletes focused on Tokyo Worlds despite Chan fever
5 Aug 2025
- Varsities VCs protest course fee cuts as debts soar to Sh85 billion