Skip to main content
Skip to main content

Viwango vya umaskini vyakatiza ndoto ya wasichana kwa changamoto ya sodo Nanyuki

  • | Citizen TV
    132 views
    Duration: 1:20
    Viwango va juu vya umaskini katika kaunti ya Laikipia vinazidi kutatiza elimu kwa mtoto msichana hivi kwamba baadhi yao hushindwa kusoma kwa kukosa fedha za kugharamia bidhaa muhimu kama sodo. Mwakilishi wa kike katika kaunti hiyo Jane Kagiri aamesema kwamba kuna baadhi ya maeneo ya Laikipia ambako wasichana hutumia majani ya miti ama nguo kuu kuu nyakati zao za hedhi jambo ambalo linalowashusha hadhi sana wanafunzi wa kike. Kagiri amesema kwamba kupitia hazina ya NGAAF sodo zitatolewa katika shule zote 290 zilizoko Laikipia ili kuhakikisha kwamba mtoto msichana amepata nafasi sawa na mtoto wa kiume kuhudhuria masomo.