- 2,226 viewsDuration: 1:21Vuguvugu la vijana wanachama wa ODM wameunga mkono wito wa kinara wa chama Dkt. Oburu Odinga wa kufanya mazungumzo ili kutatua migawanyiko katika chama hicho. Wakizungumza mjini Machakos, vijaa hao walisisitiza kujitolea kwa kwao katika kuendeleza mazungumzo na utangamano huku wakisema kuwa malumbano yanayoshuhudiwa yanaweza kusambaratisha chama hicho. Kwa sasa, vuguvugu hilo linaunga mkono hatua ya kutaka kuwaondoa baadhi ya wanachama wanaodaiwa kuasi chama na kusababisha malumbano. Vijana hao pia wanasema wanaunga mkono hatua ya vigogo wa ODM ya kutaka kushirikiana na UDA katika uchaguzi mkuu ujao.