Waakilishi wa wadi Kericho wadai udukuzi Kwenye kura ya kumng’oa Gavana Mutai, warekodi taarifa DCI

  • | Citizen TV
    339 views

    Waakilishi wadi 18 kutoka kaunti ya Kericho wamefikisha taarifa katika Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kuhusiana na madai kwamba watu wasio waakilishi wa bunge hilo walihusishwa na upigaji kura wa kumbandua mamlakani Gavana Erick Mutai kwa kutumia akaunti zao za kielektroniki.

    Wakizungumza baada ya kuandikisha taarifa, waakilishi hao walidai kundi la watu wasiojulikana liliingia kwa kutumia jumbe zao za kibinafsi na kushiriki upigaji kura kupitia mfumo wa kielektroniki wa bunge. Aidha, wamesema sasa wanahofia usalama wao. Waakilishi hao wamepinga vikali matokeo ya kura hiyo wakisisitiza kuwa kanuni za bunge hilo zinatoa nafasi ya njia mbadala ya upigaji kura.