Waakilishi wadi watatu katika bunge la kaunti ya Narok wamechukua nyadhifa zao mpya, baada ya kuchaguliwa na bunge la kaunti hiyo, akiwemo kiongozi mpya wa wachache bungeni humo..
Hii ni kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu ya kumuondoa Wilson Murkuya kama kiongozi wa wachache pamoja na nafasi zingine mbili. Wakizungumza jana jioni nje ya majengo ya bunge hilo watatu hao wakiongozwa na kiongozi mpya wa wachache Salash Kisotu wameahidi kuwajibika serikalini bila uoga au mapendeleo.
Francis Ole Kuyioni ambaye ni mwakilishi wadi ya Nkareta akichaguliwa Kiranja mkuu huku Kimiti Lemiso ambaye ni mwakilishi Wadi ya Kekonyokie akiidhiinishwa kuwa mwanachama wa bodi ya utendakazi. Mwingine ni Daniel Kilerai, mwakilishi wadi ya Majimoto aliyepata wadhfa wa naibu mwenyekiti wa walio wachache.