- 195 viewsIkiwa ni miezi tisa tangu vita kuanza huko Gaza, waandamanaji wa Israeli waliziba barabara kuu kote nchini humo Jumapili, wakimtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujiuzulu na kushinikiza sitisho la mapigano ili kuwarejesha mateka kadhaa wanaoshikiliwa na Hamas. Maandamano hayo yamekuja huku juhudi za muda mrefu za amani zikipamba moto wiki iliyopita wakati Hamas ilipoachana na dai lake kuu kwa Israeli kuahidi kumaliza vita hivyo. Kikundi cha wanamgambo bado kinataka wapatanishi kuhakikisha sitisho la kudumu la mapigano, wakati Netanyahu ameapai kuendelea na mapigano mpaka Israeli itakapo angamiza uwezo wa kijeshi na utawala wa wanamgambo wa Hamas. “Makubaliano yoyote yatairuhusu Israel kurejea na kupigana mpaka malengo yake ya kivita yafanikiwe,” Netanyahu alisema katika taarifa yake Jumapili ambayo ilikuwa na uwezekano wa kuongeza wasiwasi kwa Hamas kuhusu pendekezo hilo. “Siku ya Usumbufu” ya Jumapili ilianza saa 12:29 asubuhi , wakati huo huo ambapo wanamgambo wa Hamas waliporusha roketi za kwanza kuelekea Israel Oktoba 7 na kuchochea vita. Waandamanaji waliziba barabara kuu na kukusanyika nje ya makazi ya mawaziri wa serikali. Karibu na mpaka wa Gaza, waandamanaji wa Israeli walirusha Maputo 1,500 ya rangi nyeusi na njano kuashiria kuuawa na kutekwa kwa raia wenzao. Hannah Golan alisema alijitokeza kupinga “kutelekezwa kwa jamii zetu kunakofanywa na serikali yetu.” Aliongeza kuwa: “Ikiwa ni miezi tisa leo, katika siku hii yenye nuksi, na bado hakuna yeyote katika serikali yetu anaye wajibika.” Wanamgambo wa Palestina waliwauwa takriban watu 1,200 katika shambulizi la kushtukiza na kuwachukua mateka wengine 250. Shambulizi la kulipiza kisasi la Israel limeuwa zaidi ya Wapalestina 38,000, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo hilo, hesabu yao haitofautishi kati ya wapiganaji na raia. - AP #Haifa #waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen
Waandanamanaji washinikiza Netanyahu ajiuzulu na mapigano yasitishwe
- - Kenya-Finland Ties ››
- 14 May 2025 - Safaricom CEO Peter Ndegwa has addressed concerns about the company's involvement in the Social Health Authority (SHA) system, clarifying that its role is limited to the digitisation of the process.
- 14 May 2025 - Sean "Diddy" Combs' former girlfriend, Casandra Ventura, the star prosecution witness at the hip-hop mogul's sex trafficking trial, testified on Tuesday that her music career began to suffer as she increasingly spent her time participating in days of…
- 14 May 2025 - Senators yesterday put Kericho Governor Dr Eric Mutai on the spot over stalled Early Childhood Development and Education (ECDE) classroom projects, some of which have remained incomplete since the onset of devolution. This even as the lawmakers…
- 14 May 2025 - South Africa's unemployment rate rose in the first quarter of this year, with statisticians fretting that increasing numbers of people appear to have given up looking for work.
- 14 May 2025 - Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu said the military will enter Gaza "with full force" in the coming days, despite ongoing ceasefire efforts and the release of a US-Israeli hostage from the war-ravaged territory.
- 14 May 2025 - Finland President Alexander Stubb has hailed the historical Kenyan Gen Z movement witnessed in June last year during the anti-government protests, saying it was a momentous display of democracy.
- 14 May 2025 - The 20,000 intern teachers employed by the Teachers Service Commission (TSC) will have to work on a temporary basis for at least two years after the commission was denied budgetary allocations to employ them on permanent and pensionable terms. The…
- 14 May 2025 - Opposition leaders are now claiming that the Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) nominees presented to Parliament for approval to take up management of the electoral body are a project to rig the 2027 General Election.
- 14 May 2025 - CBK rejects banks' rate cap claims, digs in on Ruto's loan reforms
- 14 May 2025 - How current political ongoings might affect various 'kingpins'