- 199 viewsWaasi wa kikundi cha Hayat Tahrir al-Sham (HTS) wamesema walikuwa wameikamata miji ya Syria ya Talbis na Rastan. Hatua hiyo imewafikisha ndani ya kilometa kadhaa karibu na mji wa Homs, kanda za video katika mitandao ya kijamii Ijumaa (Desemba 6) zinaonyesha kile kilichosemwa ni waasi wakipita na magari katika mji wa Rastan. Kanda ya video hiyo iliyochukuliwa kutoka juu ya jengo moja, iliwaonyesha wapiganaji hao wakipita na magari na pikipiki wakifyatua risasi hewani kusherehekea wakati msafara huo ulipopita mjini humo. Shirika la Habari la Reuters liliweza kuthibitisha eneo hilo kuwa ni Rastan, mji ulioko takriban kilomita 20 kaskazini mwa Homs, kutokana na mpangilio wa mitaa, majengo, mnara wa msikiti na mnara wa saa unaonekana kutoka mbali unaofanana na picha za satalaiti na picha za kumbukumbu. Reuters haikuweza kuthibitisha tarehe maalum video hiyo ilichukuliwa, lakini Kikundi kinachofuatilia haki za binadamu Syria kimeripoti kuwa mji huo ulichukuliwa na waasi Ijumaa (Desemba 6). Mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Russia usiku kucha yameharibu daraja la Rastan katika barabara kuu ya M5, ambayo ndiyo njia kuu kwenda Homs, kuwazuia waasi hao kulitumia kusonga mbele, afisa wa jeshi wa Syria ameiambia Reuters. Hezbollah imetuma idadi ndogo ya “vikosi vya uangalizi” kutoka Lebanon kwenda Syria usiku kucha kuwasaidia kuzuia waasi wanaipinga serikali kuukamata mji wa kimkakati wa Homs, maafisa wawili wa ngazi ya juu w wa Lebanon wameiambia Reuters. Afisa wa jeshi la Syria na maafisa wawili wa kanda ambao wako karibu na Tehran pia wameiambia Reuters kuwa vikosi maalum kutoka kikundi kinachoungwa mkono na Iran, Hezbollah walivuka kutoka Lebanon na kuingia Syria usiku kucha na wameanza ulinzi wa Homs. - Reuters #waasi #hayattahriralsham #syria #tablis #rastan #hezbollah #iran #voa #voaswahili
Waasi wa Hayat Tahrir al-Sham waiteka miji miwili chini ya serikali
- - NSL promotion race ››
- 18 Jun 2025 - KNCHR has recorded 22 casualties during the Tuesday demonstrations calling for the resignation of Deputy Police Inspector General Eliud Lagat over his alleged involvement in teacher Albert Ojwang's murder.
- 18 Jun 2025 - Today’s protests took a sinister turn as police officers and hired thugs joined forces in plain sight. In a scene both brazen and unsettling, hired goons arrived on motorbikes, others armed with clubs and whips terrorizing innocent passers-by all under…
- 17 Jun 2025 - What had been intended as protests to demand accountability over the murder of teacher Albert Ojwang in police custody last week turned into an all-out clash pitting three groups: the police, protesters and hired goons.
- 17 Jun 2025 - The police officer who shot an unarmed mask vendor during the demonstrations held in Nairobi on June 17, 2025, has been arrested.
- 17 Jun 2025 - At around 10 p.m. on a cold night, a sudden sharp pain on the right side of her stomach sent 22-year-old Vestina Samson to the ground. Writhing in pain, Vestina’s family was unsure how to help her.
- 17 Jun 2025 - Three officers, among them the Officer Commanding Station at Mawego Police Station, where the late Albert Ojwang’ was briefly held before his controversial transfer to Nairobi, have now recorded statements as investigations gather pace.
- 17 Jun 2025 - The streets of Nairobi on Tuesday were nothing short of lawless as police officers worked with goons to fight off protesters.
- 17 Jun 2025 - Gachagua decried the excessive use of force by police during protests
- 17 Jun 2025 - “The nation is reeling from the deeply troubling shooting of an unarmed civilian.”
- 17 Jun 2025 - The tragic road accident along the Bondo-Kisian road also left 30 others injured