Nani atapeperusha bendera ya urais ya ACT?

  • | BBC Swahili
    1,951 views
    Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo imetangaza majina mawili ya watakaowania nafasi ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu Tanzania. Chama hicho kimewataja Aaron Kalikawe na ⁠Luhaga Mpina. Kwa upande wa Urais wa Zanzibar Halmashauri Kuu imependekeza jina la Ndugu Othman Masoud Othman ambaye ndiye mwanachama pekee aliyechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo. Majina ya wagombea yaliyopendekezwa yamewasilishwa katika Mkutano Mkuu Taifa kwa ajili ya kupigiwa kura. Ni Ipi hatima ya siasa za uchaguzi nchini Tanzania? @RoncliffeOdit anaangazia hili na mengine Mengi leo saa tatu usiku katika Dira ya Dunia TV, itakayokujia mubashara kupitia ukurasa wa YouTube BBC Swahili. #bbcswahili #tanzania #siasa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw