Skip to main content
Skip to main content

Waathiriwa wa bomu la 1998 Kenya wanyimwa fidia

  • | BBC Swahili
    18,073 views
    Duration: 1:07
    Mahakama Kuu ncini Kenya imetupilia mbali ombi la kutaka kulipwa kwa wahanga wa mlipuko wa bomu wa mwaka 1998 uliotokea jijini Nairobi, ikiamua kuwa waombaji walishindwa kuthibitisha kuwa serikali ilipuuza wajibu wake wa kuzuia shambulio hilo. Katika hukumu iliyotolewa leo Jumatano, Jaji Lawrence Mugambi aliamua kwamba ombi hilo, lililowasilishwa mwaka 2021, halina umuhimu na halikuthibitisha uwajibikaji kwa upande wa serikali. Hii imewaacha wapi maelfu walioathirika na shambulizi hilo la kigaidi lililotokea Nairobi na Dar es Salaam? @RoncliffeOdit atakuwa na maelezo zaidi katika Dira ya Dunia TV saa tatu usiku kwenye ukurasa wetu wa YouTube BBC Swahili. #bbcswahili #kenya #tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw