Waathiriwa wa mafuriko Isiolo wapewa msaada na serikali ya kitaifa

  • | Citizen TV
    147 views

    Familia zilizoathiriwa na mafuriko katika eneo la Ngaremara, kaunti ya Isiolo sasa zimepata afueni baada ya serikali ya kitaifa kuwapa chakula cha msaada, vyandarua na shillingi milioni 37. Familia hizo zilihamia maeneo salama katika shule ya upili ya wavulana ya Ngaremara baada ya mvua inayoendelea kusomba nyumba na mali zao.