Skip to main content
Skip to main content

Waathiriwa wa mafuriko Namanjalala wataka wahamishiwe mahali salama

  • | Citizen TV
    327 views
    Duration: 2:02
    Wakazi wa eneo la Namanjalala, kaunti ya Trans Nzoia, walioathiriwa na mafuriko wanatoa wito kwa serikali kuwatafutia makazi mbadala, wakisema eneo hilo halikaliki. Wakizungumza baada ya kupokea msaada wa chakula na malazi uliotolewa na Mwakilishi wa kike kaunti hiyo, Lillian Siyoi, wakazi hao walisema kuwa wako tayari kuhama eneo hilo iwapo serikali itawapatia ardhi mbadala na salama ya kuishi . familia zaidi ya elfu mbili zimeripotiwa kuathirika katika eneo hilo, huku wengi wakikosa makazi, chakula na mahitaji muhimu ya msingi.