Waathiriwa wa mafuriko nchini wakabiliwa na hali ngumu

  • | Citizen TV
    260 views

    Huku idara ya utabiri wa hali ya anga ikionya dhidi ya ongezeko la mvua na dhoruba kali katika sehemu mbali mbali nchini, waathiriwa wa mafuriko wameendelea kukumbwa na wakati mgumu kwenye kambi zao za muda. Kulingana na takwimu za shirika la msalaba mwekundu zaidi ya watu elfu themanini na saba wamekosa makao huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka.