Wabunge 10 Wanawake kutoka Mlima Kenya wahofia kuchipuka tena kwa kundi la Mungiki

  • | West TV
    222 views
    Zaidi ya wabunge 10 wanawake kutoka eneo la mlima kenya wamejitokeza kutoa lalama zao kuhusu hali ambapo wanahofia huenda kundi haramu la mungiki lililoongozwa na aliyekuwa kiongozi wake maina njenga limeanza kufufuliwa katika eneo hilo ambapo vijana wanadaiwa kusajiliwa kwenye kundi hilo lililosababisha maafa ya mamia ya wakenya na kupotea kwa mali miaka ya hapo awali Wabunge hao wakiongozwa na mbunge mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya nyandarua faith wairimu, waliambia wanahabari katika majengo ya bunge la taifa kwamba wana hofu kubwa kufuatia mienendo inayoanza kushuhudiwa katika eneo hilo ambapo wakazi wanatishiwa na hata kushambuliwa huku vjana wao wakishawishiwa kujiunga na genge hilo